Chanzo cha Virusi vya Corona

Mlipuko wa virusi vya corona ambao umewawacha zaidi ya watu milioni moja wakiwa wameambukizwa na wengine 60,000 wakiwa wamefariki umebadilisha ulimwengu ulivyokuwa.

Na pengine kwa sababu ya athari yake kubwa umezua msururu wa nadharia zilizozuka punde baada ya visa vya kwanza kutangazwa nchini China mapema mwezi Januari.

Wengi wao wanaangazia nadharia mbili: Ya kwanza ni kwamba virusi hivyo vya corona vilitengenezwa katika maabara moja ya China na kusambazwa kama silaha ya kibaiolojia dhidi ya mataifa yenye uwezo mkubwa. Na sababu ya pili ni kwamba kirusi hicho kilifanikiwa kutoroka kutokana na uzembe wa watafiti wa China na hivyobasi kuanza kusambaa kote duniani.

Wale wanaowatetea wanasema kwamba kuna virusi vinavyotengezwa na chemikali kwa lengo la kufanyiwa utafiti wa kisayansi na kwamba hapo kale vimekuwa vikivuja katika maabara zinazodaiwa kuwa na usalama wa hali ya juu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *