Joe Biden sasa ndiye rais wa Marekani

Ni rasmi kwamba Hatimaye Joe Biden amekula kiapo na kuwa rais wa 46 wa taifa la Marekani hafla ambayo imefanyika mbele ya jaji wa Mahakama Kuu John Roberts.

Baada ya kula kiapo Biden amelihutubia taifa kwa mara ya kwanza akiwa Rais wa Marekani akisema ambapo ametaja siku hii kama ya kihistoria na matumaini kadhalika mwanzo wa demokrasia komavu.

Amesisitiza umuhimu wa kudumisha umoja katika juhudi za kukabili changamoto ambazo zinazolikumba taifa hilo lenye uwezo mkubwa kiuchumi huku akiwaomba raia wote kuungana naye ili kuafikia ndoto hiyo.

Mtangulizi wake, Donald Trump hajahudhuria tukio hilo muhimu, na hatua hiyo imemfanya kuwa rais wa kwanza kutohudhuria sherehe za kuapa kwa mrithi wake tangu mwaka 1869.

Makamu wa Rais mteule Kamala Harris aliapishwa mbele ya Biden – kuwa mwanamke wa kwanza na mtu wa kwanza mweusi na mwenye asili ya Asia na Amerika aliyeinuliwa kuhudumu katika nafasi ya pili muhimu baada ya Urais.

Shughuli za uapisho zimefanyika wakati kukiwa na ulinzi mkali baada ya waandamanaji wanaomuunga mkono Trump kufanya vurugu tarehe 6 mwezi Januari.

Wanajeshi 25,000 wanalinda eneo linalofanyika sherehe hizo, sherehe ambazo zimekosa kuhudhuriwa na maelfu ya watu kama ilivyo desturi yake kwa sababu ya janga la corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *