TSC; Walimu wakuu hawatastaafu hadi wawajibikie pesa za shule

Wizara ya elimu imeendelea kuonya dhidi ya ubadhirifu wa fedha katika shule za umma, walimu wakuu wanaotarajia kustaafu wakionywa kuwa hawataruhusiwa kuondoka hadi wahakikishe kuwa wanawajibikia matumizi ya fedha katika shule hizo.

Akiwahutubia walimu wakuu katika maeneo ya Webuye Magharibi na Mashariki  katika kaunti ya Bungoma, kwenye warsha ya mafunzo ya matumizi ya fedha, afisa  wa tume ya huduma ya  walimu TSC kule Webuye Mashariki Kennedy Mukenye na mkurugenzi wa elimu katika eneo hilo Linda Sereti, wametoa wito kwa walimu, kuhakikisha kuwa fedha zinazoelekezwa katika shule hizo zinatumiwa ifaavyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *