WHO yatahadharisha kuhusu Ebola Uganda

Mkuu wa shirika la afya duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema Jumanne kwamba ana wasiwasi mkubwa na mlipuko wa ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao umeenea hadi Uganda.

Akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa wa afya mjini Geneva, mkuu wa shirika la afya duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kwa sababu nina wasiwasi mkubwa kuhusu ukubwa na kasi ya janga hili, tutaitisha kikao cha kamati ya dharura leo ili kutushauri kuhusu mapendekezo ya muda. Kufikia sasa, visa 30 vimethibitishwa nchini Kongo kutoka mkoa wa kaskazini wa Ituri.

Afisa wa WHO alionya Jumanne kwamba muda wa mlipuko mbaya wa ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unaweza kuwa mrefu. 

Anne Ancia, mwakilishi wa WHO wa Kongo alisema hadhani kama katika miezi miwili watakuwa wamemaliza mlipuko huu.

Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Geneva, akizungumza kutoka Bunia katika eneo la Ituri nchini Kongo, akizungumzia mlipuko wa hivi karibuni wa ebola ambao ulichukua miaka miwili.

Wakati huo huo, shirika la kudhibiti na kuzuia magonjwa barani Afrika, Africa CDC, limetangaza mlipuko wa ugonjwa wa ebola nchini Kongo na Uganda kuwa dharura ya afya ya umma ya bara zima katika taarifa iliyotolewa Jumatatu jioni.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imerekodi vifo 131 kutoka kwa visa 513 vinavyoshukiwa vya Ebola na kumekuwa na kifo kimoja katika nchi jirani ya Uganda.

Wakati haya yakiarifiwa, wizara ya afya ya Ujerumani mesema hivi leo kwamba Ujerumani inajiandaa kumlaza na kumtibu raia wa Marekani aliyeambukizwa ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *