Wakaazi wanaoishi kandokando ya msitu wa Kaptagat katika kaunti ya Elgeiyo Marakwet, wameelezea kuridhishwa kwao na uamuzi wa mahakama wa kusimamisha kwa muda shughuli za kuwekwa kwa uzio wa kuzunguka msitu huo.
Wakaazi hao walikuwa wamefika mahakamani wakipinga kuwekwa kwa uzio huo wa umeme, wakisema kuwa unakiuka haki zao za matumizi ya msitu huo, na kwamba hawakuhusishwa kwenye maamuzi ya kuwekwa kwa uzio huo.
Haya yanajiri baada ya naibu rais Kithure Kindiki juma moja lililopita, kusema kuwa wakaazi hao watapewa lango la kuingia kwenye msitu huo, swala ambalo wakaazi hao wamepuuza.
Wakaazi hao kadhalika wamewashutumu baadhi ya wanasiasa wanaotoka katika eneo hilo kwa kutumia pesa nyingi za kuandaa hafla kubwa za kupanda miche, kisha kuondoka na kuziwacha zikinyauka.
