Askofu Simon Peter Kamomoe amesimikwa kuwa askofu wa pili wa Jimbo katoliki la Wote, baada ya askofu wa kwanza wa Jimbo Hilo Paul kariuki Njiru kustaafu.
Akihubiri katika maadhimisho ya Misa ya kusimikwa kwa askofu Kamomoe, askofu mwandamizi wa Jimbo katoliki la Machakos Joseph Mwongela ametoa wito kwa familia kuwa na upendo na kusemezana Kila siku, kama njia Moja ya kudumisha amani, kwa kuwa familia ndio msingi wa miito mbalimbali kanisani.
Askofu Mwongela ametoa wito kwa familia kushikana na kuvumilia changamoto mbalimbali, kwa kuwa kile mwenyezi Mungu ameandaa kitatimia kwa binadamu.
Amewataka viongozi wa kisiasa nchini kuwapa wananchi kile ambacho kinafaa sio kile ambacho wanakihitaji, kwa kuwa huduma Bora ndio hukuza mshikamano wa kitaifa.
Amewahimiza watendakazi katika shamba la bwana kuwa wavuvi wa watu Bali sio wavuvi wa Mali na tamaa ya Dunia hii ambayo imejaa kelele nyingi
Askofu Simon Peter Kamomoe aliteuliwa kuwa askofu msaidizi wa Jimbo kuu katoliki la Nairobi na baba mtakatifu Francisco, Kisha akateuliwa kuwa askofu msaidizi wa Jimbo katoliki la Wote Kisha askofu msimamizi na hatimaye askofu wa pili wa Jimbo Hilo.