Maafisa wa usalama eneo la Kerio Valley kaunti ya Elgeyo Marakwet,wameanzisha msako mkali dhidi ya biashara ya pombe haramu katika eneo hilo
Akiongoza zoezi hilo,naibu kamishna wa Kerio Valley Peter Lekitashar,amesema kuwa kupitia ushirikiano wa wakazi wa eneo hilo,wameweza kufanikisha oparesheni hiyo
Wakazi wa eneo hilo wamepongeza juhudi hizo za serikali wakisema kuwa biashara ya pombe haramu katika eneo hilo imechangia pakubwa vijana wengi kuwa waraibu wa pombe haramu na matumizi ya dawa za kulevya