Makleri na majandokasisi wametakiwa kufahamu fika jukumu walilotwikwa na mwenyezi Mungu, ni kuongoza Kundi lake Kwenda mbinguni kwa kuwa karibu nao na kuwasikiliza.
Askofu wa jimbo katoliki la Nakuru Cleophas Oseso Tuka ametoa wito kwa mapadre kufahamu fika jukumu lao la uinjilishaji kwa kujisadika bila kujibakisha, akisema kuwa siku zote uwepo wao karibu na wakristu ndio utakayowapa hekima ya kuwaongoza na kuwasikiliza waumini walio na changamoto mbalimbali.
Amewataka mapadre kuwa kimbilio la kuwapa wale waliovunjika moyo matumaini, akitoa wito kwa wakristu kadhalika kuwaombea mapadre kila siku, kwa kuwa hata wao siku zote shetani huwawinda, kutokana na kuubeba ujumbe wa kristu, kwa kuwa kumwinda mtumishi wa ni kuangamizi wana wa Mungu.
Askofu Oseso amewakanya wakristu dhidi ya kuwashurutisha na kuwakashifu mapadre hao kila wanapoteleza kwa kuwa wao kadhalika ni binadamu, akitoa wito kwa wakristu siku zote kuwapa muda wa kupumzika na kuwatia moyo kwa ajili wa uenezwaji wa injili.
