ukatili

Mwanamke mmoja amefikishwa mahakamani Eldoret na kufunguliwa mashtaka ya kumfanyia ukatili mpwa wake mwenye umri wa miaka 11.

Benadine Jepkemoi cherotich akiwa kama mlezi wa mtoto huyo anadaiwa kumchapa na kumsababishia majeraha kati ya tarehe tofauti mwezi Novemba mwaka wa 2025 na mwezi mei mwaka huu katika mtaa wa kapsoya katika kaunti ya Uasin Gishu.

Cherotich alikanusha mashtaka dhidi yake alipofikishwa mbele ya hakimu mkaazi wa mahakama ya Eldoret Odhiambo Gweno

Gweno aliamuru mshukiwa huyo kuzuiliwa kwenye rumande ya gereza la Eldoret hadi tarehe 22/5/2026 ambapo mahakama itaamuru kuhusu ombi lake la kutaka aachiliwe kwa dhamana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *