Magufuli Aapishwa

Jamuhuri ya muungano wa Tanzania tayari imemuapisha John Pombe Magufuli kuwa rais wa taifa hilo kwa awamu ya pili.

Rais Magufuli ametetea nafasi yake baada ya kushinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28.10.2020.

Magufuli alishinda kwa kupata kura 12,516,252 ambayo ni asilimia 84 ya kura zote zilizopigwa. Tundu Lissu kutoka chama cha upinzani cha Chadema ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 1,933,271 ya kura zote ziizopigwa.

Jumla ya watu 15,91950 walipiga kura hizo wakati waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 29,754,699 kwa mujibu wa Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC).

Hii ni awamu ya pili kwa rais Magufuli kuongoza Tanzania, yeye ndiye alikuwa rais wa tano kuiongoza Tanzania kuanzia mwaka 2015 mpaka 2020. Na sasa anatarajia kuongoza mpaka mwaka 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *