Kaunti ya Uasin Gishu yaweka mikakati ya kukabili mafuriko

Serikali ya Kaunti ya Uasin Gishu, imeimarisha hatua zake za kukabiliana na mafuriko katika maeneo yaliyotambuliwa kukumbwa na mafuriko ili kuwaepusha wakazi dhidi ya hasara na uharibifu wa mali.

Kulingana na waziri wa barabara kwenye kaunti hiyo mhandisi Joseph Lagat, kaunti hiyo imekuwa ikifanya kazi mfululizo katika miradi ya kufungua mifereji ya maji, ujenzi na madaraja, ufunguzi wa njia za kupitishia maji zilizoziba na uchimbaji wa mitaro ili kuongeza mtiririko wa bure wa maji yanayofurika.

Aidha, wakazi wamehimizwa kupiga ripoti kwa idara husika wanaposhuhudia hali yoyote ya dharura ili kupata usaidizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *