Hamasisho dhidi ya Malaria Elgeiyo Marakwet

Serikali ya kaunti ya Elgeyo Marakwet kupitia wizara ya afya inaendeleza hamasisho kuhusu namna ya kudhibiti ugonjwa wa malaria.

Kulingana na Afisa mkuu wa afya katika kaunti hiyo Caroline Magut, kaunti hiyo ni miongoni mwa kaunti ambazo zimeathirika na Malaria katika eneo la kaskazini mwa bonde la ufa.

Magut ametoa wito kwa wakazi kutumia vyandarua vya kuzuia mbu kama njia mojawapo ya kudhibiti Malaria miongoni mwa mbinu zingine akidokeza kuwa msimu wa mvua huchangia pakubwa kuzaana kwa mbu.

Aidha, ametaja ukosefu wa uhamasisho wa kutosha kwa wenyeji kuhusu namna ya kuzuia ugonjwa wa Malaria na pia serikali kukosa mpango wa kusambaza neti za kuzuia mbu kwa wananchi wasio kwenye kitengo cha mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano, kama changamoto kuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *