Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret,ameongoza misa ya pasaka katika kanisa la moyo mtakatifu wa yesu kathedrali huku wakristu wakifuatilia misa hiyo kwenye kituo hiki cha Upendo Fm.
Kinyume na maelfu ya wakristu ambao hukusanyika katika misa hii,waliohudhuria ni baadhi ya mapadre wanaofanya kazi katika afisi za jimbo na wale wanaoishi na askofu,huku idadi ikiwa ni watu wasiopungua 10.
Katika homilia yake,askofu amewahimiza wakristu kutangaza habari njema ya ufufuko wa kristu kwa kuwasaidia maskini.
Askofu amewatia moyo wakristu kwamba wasiogope kwani kwa ufufuko wa kristu,yote yawezekana,huku ujumbe wake wa pasaka ukiwa kuwa wenye msaada katika jamii.
Askofu pia amewasilisha heri zake za pasaka kwa wakristu wote jimboni na viongozi wa serikali za kaunti.