Vijana Nandi wamehimizwa kutolaza damu

Wito umetolewa kwa vijana katika kaunti ya Nandi kutotegemea vya bwerere ila wajikaze kisabuni katika juhudi za kujijengea maisha bora siku za baadaye.

Ni kauli yake kamishna wa kaunti hiyo Wiberforce Kilonzo ambaye amesikitikia kuongezeka kwa visa ambavyo vijana wamelaza damu na kusubiri urithi kutoka kwa wazazi wao, swala hili akisema sharti likomeshwe mara moja.

Kamishna huyo amewataka wazazi nao kuwaripoti wanao ambao kwa njia moja au nyingine huenda wakawadhulumu ili waweze kupewa adhabu kwa mujibu wa sheria za nchi.

Kauli yake kamshina huyo ikungwa mkono na afisa msimamizi wa upelelezi kaunti hiyo ya CCIO Peter Ochieng ambaye amewataka vijana kujituma kazini ili kuweka matumaini ya maisha bora kesho kuwa hai.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *