Jengo la St John amani center Lawekwa wakfu na askofu mkuu Kimengich

Askofu mkuu mwandamizi mteule Dominic Kimengich amelibariki jengo la St John’s amani center, na kuweka wakfu kama mradi wa Jimbo katoliki la Eldoret.

Katika hafla hiyo askofu mkuu mwandamizi mteule Kimengich amesema kuwa jengo Hilo litakuwa kitega uchumi katika Jimbo la Eldoret, akiwashukuru wakristu Pamoja na kamati ya kusimamia ujenzi huo  kwa kujitolea kwao katika mradi huo, akisema kuwa ujenzi huo ulifanywa  kwa uadilifu wa hali ya juu.

Askofu mkuu Kimengich ameweka wakfu jengo wakati ambapo anasherehekea miaka arobaini kama padre na miaka sita kama mchungaji wa Jimbo la Eldoret.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *