Ukuruba baina ya kanisa na viongozi ndio chanzo cha amani Kerio

Gavana wa kaunti ya Elgeiyo Marakwet Welsey Rotich amepongeza ushirikiano wa kanisa katoliki na serikali ya gatuzi na ile ya kitaifa, katika harakati ya kurejesha amani kwenye bonde la Kerio.

Akizungumza katika hafla ya kusherehekea miaka sita ya utumishi wa askofu mkuu mwandamizi mteule Dominic Kimengich, gavana Wesley amesema kuwa amani imerejea kwenye bonde la kerio, kutokana na ukakamavu na bidii aliyokuwa nayo askofu Kimengich pamoja na ushirikiano baina ya viongozi wa kidini na wale wa kisiasa.

Kauli yake imepigwa jeki na aliyekuwa waziri Lina Jebii Kilimo ambaye amesifia utulivu ambayo unashuhudiwa kwa sasa kwenye bonde hilo, akisema kuwa askofu Kimengich ni askofu mkakamavu ambaye hakukata tamaa hata wakati wa changamoto mbalimbali zilizoshuhudiwa kwenye bonde hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *