Askofu wa Jimbo hili katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amesema kuwa Jimbo hili liko tayari kusaidia serikali kuu kuona kuwa amani imerejea katika eneo la kerio valley kufuatia visa vya uhalifu vinavyoendelea kushuhudiwa na watu kupoteza maisha.
Akiongea kwenye hafla ya ufunguzi wa kanisa katoliki la St Peters Kipsoen katika parokia ya Chelingwa eneo bunge la keiyo kaskazini kaunti ya Elgeyo Marakwet, Askofu Kimengich amesema kuwa utovu wa usalama katika eneo hilo limerudisha nyuma maendeleo.
Hata hivyo Kimengich ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa kisiasa wawe vielelezo Kwa kuhubiri amani na kuwaunganisha jamii hasa nchi inapoelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.