idara ya usalama katika kaunti ndogo ya soy kaunti ya uasingishu inaendelea kupanga mikakati ya kuimarisha usalama eneo hilo kuhakikisha hakutashuhudiwa ghasia kabla wakati wa na baada ya uchaguzi mkuu ujao.
akizungumza kwenye mkutano wa amani eneo la moisbrige kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya soy nehemiah bittok amesema tayari wametambua sehemu ambapo ghasia hushuhudiwa akisema wamekamilisha mipango ya kuimarisha usalama kuhakikisha hali ya utulivu itaendelea kushuhudiwa.
akizungumza kuhusu visa vya utekaji nyara hasa kwa watoto ambavyo vimeshuhudiwa eneo hilo bittok amesema hatua kali zitachukuliwa. dhidi ya washukiwa ambapo amefichua baadhi yao na tayari ;wamefunguliwa mashtaka.
haya yanajiri huku kanisa katoliki likiwa mstari wa mbele kuhubiri amani katika maeneoa athirika chini ya afisi ya haki na amani cjpc.
akiongoza mkutano huo katika eneo la moisbrige mratibu katika afisi ya haki na amani samwel kosgey amewahakikishia wakenya kuwa watakuwa mstari wa mbele kama kanisa kuhubiri amani kama mikakati bora ya kuwepo kwa uchaguzi usio na vurugu ifikapo mwaka wa 2022.
kadhalika ametaka jamii ambazo zinazozana kila wakati haswa kutoka maeneo ya baringo tiaty, elgeyio marakwet na pokot magharibi kukomesha vita na kuangazia maendeleo katika jamii.