Tuwei: Dumisheni Amani kuelekea Uchaguzi mkuu

Mbunge wa Mosop kaunti ya Nandi Vincent Tuwei, ametoa wito kwa wananchi kudumisha amani na utangamano taifa linapojiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Kwenye mahojiano ya kipekee na Upendo Fm, Tuwei amewataka wakenya kutokubali kuwagawanya kwa misingi ya kikabila au mirango ya kisiasa bali wazingatie umoja ambao umedumu kwa muda sasa

Aidha mbunge huyo amewataka wanasiasa kushirikiana na viongozi wa kidini katika kuleta uwiano na utangamano kadhalika kuboresha utoaji huduma kwa wananchi huku akiwahimiza kuheshimu kanisa wakati wanapopewa nafasi ya kuwahutubia waumini.

Kuhusu janga Corona, mbunge huyo amewahimiza wananchi kuendelea kuzingatia masharti ya wizara afya ya kudhibiti msambao wa virusi vya corona licha ya kuwepo kwa chanjo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *