Ndoto ya msichana mwenye umri wa miaka 15 aliye na matatizo ya ngozi yaani zeruzeru kaunti ya nandi ya kujiunga na kidato cha kwanza mwezi ujao huenda yasitimie baada ya kudai kunyimwa nafasi katika baadhi ya shule za sekondari kutokana na maumbile yake.
Msichana huyu kwa jina winnie jelimo aliyekuwa mwanafunzi katika shule ya msingi ya ilula mjini edoret kaunti ya uasingishu na kuzoa alama ya 347 katika mtihani wa kcpe amesema kwamba aliitwa katika shule za watu walio na ulemavu wa kuona kule likoni shule anayosema hakufurahia kwani ana uwezo wa kuona na ingekuwa bora akijiunga na shule ya kawaida.
Akizungumza na wanahabari amesema amezuru shule kadha kuomba nafasi lakini amenyimwa kutokana na maumbile yake na sasa anahofia huenda hataweza kutimiza ndoto yake ya masomo.
Mamake jelimo ametaka serikali kuingilia kati kupitia wizara ya elimu ili kumsaidia mtoto wake kutimiza ndoto ya kuwa daktari.