Nelson Havi aachiliwa kwa dhamana

Rais wa chama cha mawakili nchini Nelson Havi aachiliwa huru kwa dhamana ya KSh 10,000 na anatarajiwa kujibu mashtaka dhidi yake siku ya Jumatano.

Havi anashtumiwa kwa madai kuwa alimjeruhi afisa mkuu wa chama hicho, Mercy Wambua wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa katika afisi za chama hicho jijini Nairobi siku ya Jumatatu Julai 12.

Kwenye taarifa yake aliyoandikisha katika kituo cha polisi cha Muthangari, Wambua alisema alijeruhiwa kwenye mkono wake wa kulia kufuatia makabiliano yaliyozuka katika mkutano huo ambao hakuitajika. Kwa upande wake, Havi amejitetea kwamba Wambua hakustahili kuhudhuria mkutano huo kwa sababu alikuwa kwenye likizo ya lazima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *