Familia ni kigezo muhimu cha ukuaji wa kanisa na miito mbalimbali katika ulimwengu wa sasa wenye kumtambua mwenyezi mungu.
Hii ni kauli yake askofu wa jimbo katoliki la Bungoma Mark Kadima akihubiri wakati wa hafla ya wanandoa katika parokia ya St.Teresa of Avilla Naitiri ambaye alisisitiza haja ya wakristu kupokea kwa unyenyekevu mwito wa familia ili miito mbalimbali ziweze kupaliliwa katika familia kuziweka imara miito hizo.
Vilevile askofu Kadima aliwataka wakristu hao kudumisha Imani yao na mwenyezi mungu ndipo maisha yao ya ukristu ziweze kuimarishwa na kuwa wan awa mungu.
Aidha,alisisitiza haja ya wakristu kutowahukumu wengine kwa kuwa wote ni wenye mapungufu na kuwaelekeza kwa upendo na unyenyekevu ili waweze kushiriki kikamiliu shughuli zote za kanisa na kuwa wenye mweleko bora katika maisha ya ukristu.
