Gavana wa kaunti ya Elgeyo Marakwet Alex Tolgos amesema kuwa kamwe hatabadilisha msimamo wake wa kisiasa kuhusu kumwuunga mkono kinara wa ODM Raila Odinga katika azma yake ya kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Kulingana na gavana huyo, kila mmoja ana haki ya kidemokrasia ya kumuunga mkono yeyote kwenye wadhifa wa urais pasi na kulazimishwa
Akiongea kwenye hafla ya mazishi ya mfanyibiashara mmojaMaurice Kangogo katika eneo la Kamotony, gavana Tolgos aidha, amewata wale ambao wanawania viti mbalimbali vya uongozi katika kaunti hiyo kuhubiri amani na utangamano.
Kauli yake inajiri kufuatia kuonekana kwake kwenye mikutano ya kisiasa ya Odinga alipotua maeneo ya Rift Valley.