Mbunge wa Aldai katika kaunti ya Nandi Cornelly Serem ametoa wito kwa serikali ya kitaifa kuwapunguzia wazazi karo ya shule akisema ni ghali mno.
Serem amesema kutokana na hali ngumu ya maisha, wanafunzi wengi wamelazimika kuacha shule kutokana na wazazi wao kushindwa kulipa karo.
Hata hivyo, ameitaka serikali kuingilia kati ili kuhakikisha wanafunzi nchini wanapata elimu bora ikizingatiwa kuwa ni mojawapo ya haki zao za msingi.