Iten; Mwanaume amteka nyara mtoto

Mwanamume mmoja amefikishwa katika mahakama ya Iten Kwa kosa la kumteka nyara mtoto msichana mwenye umri wa miaka 14.
Mbele ya hakimu mwandamizi Charles Kutwa Hillary Kimwetich Biwott alikabiliwa na shtaka kuwa kati ya tarehe 10/10/2021 na 17/10/2021 katika Kijiji Cha Sokoyo katika lokesheni  ya Kaptalamwa kaunti ya Elgeyo Marakwet alikuwa na nia ya kusababisha msichana huyo kufichwa kisiri na Kwa kimakosa.
Hillary alikabiliwa na kosa la pili kuwa mnamo tarehe 10/10/2021 katika Kijiji Cha Kapsarbet lokesheni ya Yemit kaunti ya Elgeyo Marakwet alimnajisi msichana huyo kinyume Cha sheria.
Hillary alipopewa nafasi ya kujitetea alikubali mashtaka hayo  huku Kiongozi wa mashtaka Judith Ayuma  akiomba korti kumpa tarehe ya kujua  ukweIi.
Hata hivyo mwanamume huyo anazuiliwa katika gereza la Tambach,kesi hiyo  ikitarajiwa kutajwa mnamo tarehe 26/10/2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *