Hofu ya Maporomoko ya ardhi Lelan

Wakazi katika kijiji cha Kaparmagai ,wadi ya Lelan katika kaunti ya Elgeyo Marakwet wanaishi kwa hofu kufuatia  maporomoko ya ardhi ambayo imeanza kushuhudiwa karibu na makazi yao.
Wakazi hao wanasema Kuwa Kuna mti mkubwa  iliyo katikati ya nyaya za umeme ambayo imeonyesha dalili za kuanguka kutokana na maporomoko hayo.
Kulingana na wakazi hao,licha ya kampuni ya kusambaza umeme nchini katika eneo hilo kujulishwa  kuhusiana na hatari ya mti huo,hawajachukua hatua yeyote hadi sasa.
Hata hivyo wametaka vitengo husika kuingilia kati na kuangusha mti huo kabla haijasababisha  hasara kubwa ikizingatiwa kuwa mvua bado ianendelea kushuhudiwa katika eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *