Baba Mtakatifu Francis Kuzuru Nchi ya Iraq

Makao makuu ya kanisa katoliki duniani – Vatican imesema kuwa Papa Francis atafanya ziara ya kihistoria nchini Iraq mwezi Machi mwaka ujao.

Katika taarifa, Msemaji wa Vatican Matteo Bruni amesema kiongozi huyo wa kanisa katoliki atazitembelea Baghdad, Mosul na Qaraqosh wakati wa safari yake iliyopangwa kuanza Machi 5 hadi 8, mwaka 2021.

Papa Francis, mwenye umri wa miaka 83 kwa muda amekuwa akizungumzia juu ya hamu ya kufanya ziara katika nchi hiyo ya Mashariki ya kati, lakini kanisa hilo limesema ziara yake itazingatia kitisho cha afya duniani.

Yeye atakuwa Papa wa kwanza kufanya ziara nchini Iraq, nchi ambayo idadi ya waumini wa Kikristo imepungua sana katika muda wa miongo miwili iliyopita.

Ziara ya Papa Francis mjini Mosul itaangaziwa zaidi hasa ikizingatiwa kuwa mji huo ulikuwa ngome ya kundi la wapiganaji wanaojiita Dola ya Kiislamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *