Makundi ya nzige yatavamia kaunti 20 kufikia katikati ya mwezi huu kulingana na shirika la umoja wa mataifa kuhusu chakula FAO
Ramani mpya imeonyesha jinsi nzige hao wanavyosafiri kutoka Somalia na Ethiopia kuingilia upande wa Kenya.
Katibu wa kudumu wa kilimo Hamadi Boga amesema nzige wachanga wanatarajiwa kufika pwani kufikia mwisho wa wiki hii .
Nzige waliokomaa tayari wamefika katika kaunti za Lamu, kilifi na sehemu za kwale na tana river.
Katibu huyo wa kudumu aliyasema hayo wakati wa mafunzo ya makundi ya watakaopambana na nzige hao kutoka Kwale, Taita Taveta, Kilifi, Makueini na Kajiado na yatasaidia kufuatilia safai za nzige hao klatika wiki tano zijazo
Upepo kutoka Somalia na Ethiopia utawafanya znige hao kusafiri upande wa kusini wakiingia Kenya.
Nzige walionekana mara ya kwanza mwaka jana disemba tarehe 28 Boga amesema .
Mwenyekiti wa shirika la mafunzo kuhusu wadudu Dr Kasina Muo amesema kenya itaanza kuvamiwa na nzoige wachanga wiki hii kisha wataongezeka katikamuda ulisalia wa disemba na januari .