Wanafunzi wa Lugulu Waandamana

Wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya upili ya wasichana ya Lugulu kaunti ya Bungoma wameandamana kulalamikia visa  vya unajisi.

Watahiniwa hao wanamshutumu mwalimu wao mkuu kwa kile wamedai ni kuwakinga washukiwa wa visa hivyo.

Wanafunzi hao wamesitisha mtihani wao wa mwigo waliokuwa wakiufanya ili kuandamana kuelezea ghadhabu zao baada ya kuibuka kuwa wasichana kadhaa wa shule hiyo wamebakwa huku mwalimu wao mkuu akishindwa kuwawajibisha washukiwa. Shunguli za kawaida zimetatizika kwa muda kufuatia maandamano hayo huku wito wao ukiwa ni washukiwa kukamatwa na kukabiliwa kisheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *