Wauguzi wa afya waingia wiki ya pili ya mgomo

Mgomo wa wahudumu wa afya unaingia wiki ya pili leo wakenya wakizidi kuhangaika kupata huduma  za matibabu haswa katika hospitali  za umma.

Wauguzi wamesisitiza kwamba kamwe hawatarejea kazini hadi pale matakwa yao yote yatakapoangaziwa na serikali  hali kadhalika serikali za kaunti.

Magavana  nao wametishia  kuwatimua wauguzi  wanaogoma na wauguzi  wanasema  maisha yao yamo hatarini haswa wakiwa  mstari wa mbele kuwahudumia wagonjwa bila vifaa vya kujiki wakati huu wa ijanga la corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *