wakristo wametakiwa kuekeza juhudi zao katika safari ya kumtambua mungu na kumkubali wakati huu wa maajilio.
katika homilia yake padre Cornelius kipchumba kwenye kanisa la moyo mtakatifu wa yesu kathedrali ametaka kila mkristo kusoma neno lake mwenyezi mungu na kungazia matendo yake kuwa mema ili yamruhusu kuingia mbinguni.
ameeleza kila mkristo kulinda imani yake kwa kuepuka majaribu ya dunia kupitia neno lake mwenyezi mungu.
hata hivvyo amewahimiza wakristo wote kukesha na kuomba ili wakati yesu anapozaliwa awapate wakiwa tayari kumpokea na kueneza injili ya kristo.