Sikukuu Ya Kristu Mfalme

Wakristo wamehimizwa kutambua kwamba wao ni wana wa Ufalme wa Mungu unaoanza hapa duniani na ukamilifu wake ni mbinguni na kwa hio Hukumu watakayoipata itatokana na matendo yao wenyewe jinsi wanavyoishi hapa duniani na kuhusiana na wenzao.

Dominika ya 34 ya mwaka A wa Kanisa kipindi cha kawaida na ya mwisho wa mwaka wa kiliturjia ikiwa ni  Kadiri ya utaratibu wa Mama Kanisa, ambapo tunaadhimisha Sherehe ya Yesu Kristo Mfalme, mfalme aliyetukomboa kutoka utumwa wa dhambi na mauti.

Katika homilia yake katika kanisa la moyo mtakatifu wa yesu hapa Cathedrali, padre Paul Peter Idiama, amewakumbusha wakristo kuwa Kristo aliye Mchungaji na Mfalme atahukumu kadiri tunavyoshuhudia imani yetu siku kwa siku na kadiri ya matendo yetu ya huruma kwa jirani.

Padre Idiama amewakumbusha wakristo kuwa hukumu yao ya mwisho inatokana na jinsi wanavyoipokea na kuiishi amri ya mapendo kwa Mungu na Jirani.

Padre Idiama amesema kuwa Upendo unaonesha kuwa jirani ni kipimo cha upendo wao kwa Mungu. Kadiri wanavyoyatendea makundi maalumu ya ndugu zao kwa mahitaji yao kama wenye njaa, wenye kiu, maskini, wageni, wagonjwa, wafungwa, na walio uchi ndivyo hivyo wanavyomtendea Kristo na ndicho kipimo cha hukumu yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *