Tuwape watoto malezi bora wakati wa janga hili la Corona

Wito umetolewa kwa  wazazi kuwaelekeza wanao na kuwapa  malezi bora wakati huu wa janga la corona.

Akiongea na idhaa hii meneja wa bodi ya filamu katika kanda mwa kaskazini  mwa bonde la ufa Emmanuel mbutu  amewataka wazazi kutenga muda na wanao na kuwapa mwelekeo bora haswa utumizi wa mitanda ili wasipotoke kimaadili.

Amesema kuwa kutokana  na utovu wa nidhamu unaoshudiwa nchini kutoka kwa baadhi ya watoto ni dhihirisho kamili kuwa wanafuatilia maswala ambayo hayastahili kwenye mitandao na pia vipindi kwenye runinga ambayo  ni ya kuyapotosha.

Ameomba  kila mtu kujukumika katika malezi ya watoto huku akisisitiza kuwa mtoto ni jamii nzima na  hivyo kuwaongoza na kuwashauri kutawafaidi pakubwa wakati huu wammesalia nyumbani kutokana na janga la corona

hata hivyo amewataka washikadau katika sekta ya mziki, vyombo vya habari na sekta zi ngine kuhakikisha ule ujumbe unawafikia watoto ni wenyw maadili ya kukubalika katika jamii.

Aidha amewashauri watoto kuttumia uhuru wao kwa makini  kwa kjiangazia upya ili wapate maisha bora siku za baadaye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *