Askofu wa jimbo katoliki la eldoret dominic Kimengich amewasihi wakristo kuendeleza kazi ya aliyekuwa askofu wa jimbo hili marehemu Askofu Cornelius Koriri kwa njia ya upendo na umoja.
kwenye homilia yake alipoongoza ibada ya misa ya kumukumbuka marehemu Askofu Cornelius Korir katika Kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu Kathedrali askofu Kimengich amesema kuwa kupitia ushirikiano kwa pamoja kutazaa matunda mema katika jamii na pia kuendeleza kazi ya mungu.
Askofu amemsifia marehemu Askofu Korir kama mwenye kukuza miito katika kanisa
huku akiwasihi mapdre kufuata nyayo zake.
Kadhalika amewataka wakristo wote kuombea familia ya marehemu kwa mungu awape nguvu wakati wa magumu yote na nchi kwa jumla iwe na amani kama ilivyokuwa mapenzi ya marehemu Korir