Juhudi za viongozi wa kanisa kuwaleta pamoja Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto huenda zikakosa kuzaa matunda baada ya wandani wao kupuuza hilo.
Kumekuwa na juhudi kutoka kwa viongozi wa kanisa kuwaleta pamoja Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.
Wandani wa naibu wa rais Ruto wameweka masharti ya kutimizwa kabla ya mazungumzo yoyote ya kumaliza tofauti za wawili hao.
Kulingana na wao, ni lazima Rais kwanza amrudishie Ruto majukumu yake ndani ya serikali iwapo anataka kuwe na mazungumzo baina yao.
Kikosi cha wabunge wa Tangatanga kilifanya kikao nyumbani kwa Ruto mtaani Karen na kusema ni lazima DP apewe heshima yake ndani ya Jubilee. Kumekuwa na juhudi kutoka kwa viongozi wa kanisa wakiongozwa na maaskofu wa katoliki kuleta Rais na DP pamoja baada ya tofauti zao kushamiri kwenye umma.