Yesu ni Mfalme wa Amani

Askofu wa jimbo la Eldoret askofu Dominic Kimengich, hii leo ameongoza misa ya dominika ya 14 ya mwaka A wa kanisa, ikiwa pia ni jumapili ambayo mama Kanisa anasherekea sherehe ya Yesu Mfalme wa Amani.

Katika homilia yake askofu Kimengich  amewakumbusha wakristu kuwa licha ya taabu na mahangaiko yanayoshuhudiwa kwa sasa kote nchini, wanastahili kufurahia katika shida kwani Mungu yuko pamoja nao kwa kila hatua wanayopiga.

Vilevile askofu pia amewakumbusha wakristu kuwa yesu pia anawafikia kupitia sakramenti takatifu inayoonyesha yupo pamoja nao huku wakijifunza kutoka kwake kwa kuwa yeye ni mnyenyekevu na mpole.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *