Mtu mmoja amethibitishwa kufariki kufuatia makabiliano kati ya magenge mawili ya kihalifu eneo la Flamingo kaunti ya Nakuru.
Inadaiwa kuwa waliotekeleza mauaji hayo walikuwa wameenda kulipiza kisasi nyumba mbili pia zikiteketezwa.
Polisi wamewatia mbaroni washukiwa 6 wanaoendelea kuzuiliwa wakisubiri kufikishwa mahakamani juma lijalo.
Kamishna wa kaunti ya Nakuru Erastus Mbui amethibitisha.