Wazazi wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwaelekeza watoto wao kwa kuwapa mashauri mema wakati huu kuna ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.
Akiongea na kituo hiki askofu wa jimbo katoliki la eldoret dominik kimengich amesema kuwa wazazi wanastahili kuongea na watoto wao kwa misingi ya kidini ili wajiepushe na makundi ambayo yanaweza kuwapotosha wakati huu shule zinazidi kufungwa.
Amewahimiza wazazi kuwa waungane na watoto wao kwa maombi wakati huu kila mtu anapitia hali ngumu ya maisha .
Hata hivyo amewatia moyo wanafunzi kuwa wawe wenye matumaini wakifuata mashauri na kuwa imani siku zote kwa vile watakuwa washindi baadaye.
