Kenya imesajili visa vipya 62 vya maambukizi ya corona chini ya saa 24, na kufikisha jumla ya visa 1,348 vya maambukizi hayo nchini.
Katibu msimamizi katika wizara ya afya Rashid Aman amesema kwamba jumla ya sampuli 2,292 zilichukuliwa chini ya saa 24, Kati ya watu hao 62, wakenya ni 59 huku wengine watatu wakiwa raia wa kigeni, umri wao ni kati ya miaka sita na 64.
Narobi ilisajili jumla ya visa 23, Mombasa 16 huku Kajiado ikisajili visa sita. Watu watatu wamepona na kuruhusiwa kurejea nyumbani na kufikisha idadi ya watu 405 waliopona ugonjwa huo nchini Aman alisisitiza umuhimu wa kupeana taarifa kamili kuhusu watu ambao muathiriwa alitangamana nao ili kusaidi katika kuwatafuta kwa lengo la kuwapa matibabu.