Mbunge mstaafu apigania maisha yake

Aliyekuwa mbunge wa Baringo Kusini Edward Kiptanui Cherotich anapigania maisha yake baada ya kushambuliwa na wezi nyumbani kwake Rongai kaunti ya Nakuru.

Edward alipelekwa hospitalini jumamosi baada ya kukatwa na shoka na wezi hao.

Kulingana na nduru za habari wezi hao waliingia nyumbani kwa Edward saa nne usiku na kuanza uvamizi wao uliokaa kwa muda wa masaa manne.

Walitekeleza uvamizi huo masaa chache baaada ya masaa ya kafyu, inadaiwa kuwa mbunge huyo alikataa na funguo za mahali pa kuweka pesa na kusababisha mvutano kati yake na majambazi hao.

Pia inadaiwa kuwa mfanyakazi wa nyumba aliweza kunajisiwa na majambazi hao na baadae kutoka na nguo za mbunge huyo na bidhaa tofauti za kibinafsi.

Inasemekana kuwa mbnge huyo yuko katika hali sawa ilhali majeraha yake makubwa yako katika mguu wake,wengi wa wasaidizi wa mbunge Edward walisema kuwa polisi hawakupatikana wakati huo wa mashambulizi hayo.

Kutoka kwetu wanajambo tunamtakia kupona kwa haraka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *