wakaazi wanaoishi karibu na bwawa la turkwel katika kaunti ya pokot magharibi wameeleza wasiwasi kuhusu kile wamesema ni kuongezeka kwa kiwango cha maji katika bwawa hilo la turkwel kutokana na mvua kubwa ambayo inaendelea kushuhudiwa katika sehemu hiyo.
wakiongozwa na mama rose chepokwo wakaazi hao wamesema bwawa hilo limefurika zaidi na huendaq likavunja kingo zake iwapo mvua itaendelea kunyesha . kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la wazee eneo bunge la pokot kusini anasema baadhi ya maafa na mikasa ambayo imekuwa ikishuhudiwa katika kaunti hiyo imekuwa ikitabiriwa tu na wazee na kutoa wito kwa serikali ya kitaifa na ya kaunti kuhakikisha kwamba hatua za mapema zinachukuliwa ili kuzuia mikasa kama hii na maafa.