watu wanaoishi na ulemavu katika eneo la disil kaunti ya kajiado wanapanga kuandamana hadi katika afisi za serikali zilizo mjini kajaido jumatano hii kushinikiza haki kutendeka hasa katika utoaji wa msaada wa serikali kwa watu wasiojiweza.
kundi hilo la watu ambalo linaongozwa na samson kutoya wanasema licha ya machifu kutikwa jukumu la kuwaandisha wale wanapaswa kupewa msaada idadi kubwa ya watu wanaoishi na ulemavu inaachwa nje na hivo wataandamana jumatano wakitaka watendewe haki. kadhalika wamemtaka kamishna wa kaunti ya kajiado johnson kanatha kuingilia kati na kuhakikisha wanapewa misaada hiyo ikizingatiwa kwa sasa wanapitia mahangaiko makubwa na hali ngumu ambayo imesababishwa na virusi vya corona.