Gavana wa Uasingishu Jackson Mandago na mwezake wa Elgeyio Marakwet Alex Tolgos wamewataka maseneta kupitisha mfumo mpya wa ugavi wa rasmali za kitaifa kulingana na idadi ya watu katika kila kaunti ili fedha zaidi zipelekwe maeneo ya mashinani.
Magavana hao wanasema kwamba mfumo huo utasaidia kaunti zilizo na idadi kubwa ya watu kupata fedha za kutosha kutoa huduma bora kwa mwananchi wa kawaida.
Naye gavana wa Busia Sospeter Ojamoong amelitaka bunge la Seneti kupitisha mswada wa ugavi wa fedha jinsi ilivyopendekezwa ikizingatiwa kaunti hiyo itanufaika na mgao wa zaidi ya shillingi milioni 500