Ndoa za mapema zachacha Narok

Baadhi ya wasichana wa kidato cha nne  mwaka huu  katika eneo la masai imara kaunti ya Narok wameolewa baada ya serikali  kutangaza kwamba shule hazitafunguliwa hadi mwaka ujao kutokana na janga la corona.

 haya ni kwa nujibu wa chifu wa eneo la aitong kaunti ndogo ya narok magharibi daniel tranky ambaye amedai kwamba wengi wa wasichana hao wamejiingiza katika ndoa kwa misingi kuwa wameshindwa kuvumilia  hadi mwaka ujao waweze kurejea shuleni.

anasema kwamba inakuwa vigumu  kuwatia mbaroni wengi wa wasichana hao kwani tayari  baadhi wamefikisha na kupitisha umri wa miaka 18.

 hata hivyo ametoa wito kwa wazazi kuwajibika kwa sana ili kuwashauri wanao kila saa ili kuepukana na ndoa za mapema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *