kina mama katika kaunti ya uasingishu wameshauriwa kuwanyonyesha wanao aghalabu miezi sita ya kwanza Hii ikiwa ni wiki ya kunyonyesha watoto.
Akiongea na kituo hiki kwa njia ya simu daktari peter barasa kutoka hospitali ya racecourse amewashauri kina mama kuhakikisha ya kwamba wanawanyonyesha wanao miezi sita ya kwanza ili kuboresha afya za watoto wao.
Amesema kuwa maziwa ya mama ina madini muhimu kwa ukuaji wa mtoto na hivyo wanapaswa kuzingatia miezi sita ya kwanza ya kuwanyonyesha wanao mfululizo.