Siku ya SECAM Kuadhimishwa

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM linaadhimisha Siku ya SECAM kuanzia tarehe 29 Julai hadi tarehe 2 Agosti 2020:

Waamini wajenge utamaduni wa kukutana na Yesu katika Neno la Sakramenti zake.

Toba na wongofu wa ndani, uwasaidie waamini kuambata utakatifu wa maisha tayari kutangaza na kushuhudia imani yao kwa Kristo na Kanisa lake.. Waamini wajibidiishe kufahamu Mafundisho Tanzu ya Kanisa ili kujenga na kudumisha umoja na mshikamano wa familia ya Mungu inayowajibika Barani Afrika. SECAM ni matunda ya maadhimisho ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, uliowahamasisha Maaskofu kutoka Barani Afrika, kushikamana kwa hali na mali, ili kuweza kukoleza ari na moyo wa kimisionari, tayari kujikita katika mchakato wa uinjilishaji wa kina, unaogusa mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *