Tiaty Baringo: Sheria kali kwa wanaoendesha tohara kwa wanawake

Maafisa katika makao ya kuwalinda wasichana dhidi ya dhulma za kitamaduni eneo bunge la Tiaty kaunti ya Baringo, wameapa kuwachukulia hatua kali za kisheria watakaopatikana wakiwapacha wasichana hao tohara.

Aidha wameahidi kuendelea kuwatunza watoto hao walioruhusiwa kurudi nyumbani kufuatia janga la korona.

Askofu mstaafu Christopher Chochoi ambaye ni msimamizi wa makao hayo eneo ya Kinyang amesema wasichana 41 waliokuwa chini yake wameruhusiwa kurudi nyumbani na wengine 10 kusalia katika makao hayo kwa kukosa pa kwenda.

Aidha amesema kumi hao wanahitaji msaada ili kujikimu katika makao hayo.

Haya yanajiri huku wanaharakati wakionya kuwa janga la corona limewaweka wasichana wengi katika hatari ya kudhulumiwa. Mwanzilishi wa shirika la Marakwet girls Ruth Kilimo amewataka machifu kuwa makini na kuhakikisha kuwa wasichana wanalindwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *