Mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo amepatikana ameaga dunia kando ya mto mmoja eneo la Sigirio katika wadi ya Kapenguria kaunti ya Pokot magharibi.
Kulingana na wakazi, mwanamume huyo huenda alisombwa na maji ya mafuriko kwani si mwenyeji wa eneo hilo.
Mwili wa mwendazake ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Kapenguria.
Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Kapenguria Julius Chimbule amewatahadharisha wenyeji dhidi ya kuvuka mito iliyofurika ili kuepuka maafa yanayotokana na mafuriko.