Seneta wa kaunti ya Narok Ledama Ole Kina, ameteuliwa mwenyekiti mpya wa kamati ya kuratibu matumizi ya pesa za umma almaarufu kama Committee on County Public Accounts and Investment (CPAIC) katika bunge la seneti.
Ledama alikuwa anamenyana na mwenzake wa Kisii seneta Sam Ongeri. Kati ya kura zilipigwa, Ledama alishinda kwa kupata kura 5 dhidi ya 4 ambazo alipata Ongeri.
Ledama kwa sasa anachukua nafasi hio kutoka kwa seneta wa Homabay Moses Kajwang ambaye alikuwa mwenyekiti wa hapo awali. Kamati hio ya wanachama tisa hushughulikia maswala ya pesa za umma katika ngazi za kaunti. Bunge la seneti limekuwa likihudumu bila mwenyekiti wake tangu mwezi disemba ilipokamilika kwa muhula ya mwenyekiti wa hapo awali.