Alhamisi kuu ishara ya huduma ya upendo

Alhamisi kuu ni siku kuu katika litujia ya kanisa ishara iliyoonyeshwa kupitia yesu kristo katika ukaristi takatifu.

Haya yamesemwa naye askofu wa jimbo la Eldoret Dominich Kimengich akisema amri hio iliofanywa mwanzo naye yesu kristo ni ishara kuu ya upendo.

Akiongea muda mfupi uliopita ndani ya idhaa hii askofu Kimengich, ameguzia kusema kuwa kulingana na sheria hakutakuwepo na maandamano ya ijumaa kuu kama ilivyodesturi huku akitoa wito kwa wakristu kufanya sala zao wakiwa majumbani.

Vilevile kufuatia mkurupuko wa virusi vya corona hapa nchini na haswa hapa mjini Eldoret, askofu Kimengich ametoa wito kwa wakristu kufuata kikamilifu kwa sheria zilizowekwa na serikali ili kuepuka kupatwa na virusi hivi na kuwatia moyo kuwa mwenyezi mungu yupo pamoja nasi katika kipindi hichi ambacho virusi hivyo vinayumbisha dunia kwa jumla

Kuhusiana na mitihani ya kitaifa ambayo inatazamiwa kusongezwa katika siku za mbeleni, askofu amehimiza kuwa muda huo uzingatiwe huku akiwataka wazazi kuwajibika zaidi katika kuhakikisha kuwa wanao wanasoma na pia kuwasaidia wazazi wao na kazi za kinyumbani huku taifa likuwa katika hali tete iwapo kutakuwepo na amri ya kutotoka nje usiku na mchana maarufu kama “lockdown”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *